23 Juni 2025 - 16:16
Hezbollah: Tuna imani na uwezo wa Iran wa kufanya Amerika na Israel kuonja kushindwa

Uchokozi huu ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na za kibinadamu, Mikataba ya Geneva, na Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambao unakataza kulenga vituo vya nyuklia na matumizi ya nguvu dhidi ya nchi huru.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon imesema katika taarifa yake: "Tunalaani vikali hujuma za kishenzi, kihayawani, na khiana za Marekani dhidi ya vituo vya amani vya nyuklia vya Iran. Ni uchokozi unaofichua sura halisi ya Marekani kama tishio kubwa zaidi kwa usalama na uthabiti wa kieneo na kimataifa." Uchokozi huu ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na za kibinadamu, Mikataba ya Geneva, na Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambao unakataza kulenga vituo vya nyuklia na matumizi ya nguvu dhidi ya nchi huru.

Tunatangaza mshikamano wetu kamili na Jamhuri ya Kiislamu, uongozi wake, na watu wake, na tuna imani kamili na uwezo thabiti na wa kweli wa Iran, na kielelezo chake cha uongozi dhabiti na shupavu, watu wake wakarimu na wapenzi, Jeshi lake la Walinzi wa Mapinduzi makini na wenye kujitolea, na vikosi vyake vya usalama na kijeshi katika kukabiliana na uchokozi huu na kumfanya adui Marekani na Mzayuni kuonja ladha kali ya kushindwa kwao, na mashambulizi yao kamwe hayawezi kuzuia maendeleo haya ya Iran.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha